Sintaksia Ya Kirai Kijalizo Na Uchopoaji Wa Viambajengo Katika Kiswahili
Abstract
Kazi hii imeshughulikia sintaksia ya Kirai kijalizo (Kkijzo) na uchopoaji wa viima katika sentensi za Kiswahili. Viambajengo katika sentensi ya Kiswahili huweza kuchopolewa kutoka kiwango cha kirai wakati (Kwkt) na kutua katika kiwango cha Kkijzo. Kutokana na wingi wa dhima za viambajengo vinavyochopolewa na kutua katika kiwango cha Kkijzo, mbali na virai vya kidesturi vya Kkijzo kazi hii imependekeza kupanuliwa kwa Kkijzo ili kijumuishe virai vya ziada kama vile: Kirai arifu na Kirai kiwakilishi. Aidha kazi hii, imechunguza mofosintaksia ya vijalizo changamano ndi- na amba- na kipatanisho kijalizo -o- kama vipashio vinavyotumika kuchopoa viambajengo katika sentensi za Kiswahili. Lengo hasa la utafiti huu ni kubaini nafasi zinazokaliwa na viambajengo hivi vya uchopoaji kwa mujibu wa muundo mzima wa sentensi zilizochopolewa. Uchanganuzi wa data katika karatasi hii utafanywa kwa kujikita kwa nadharia ya Kanuni Finyu hasa mapendekezo ya hivi karibuni ya kigezo cha ugandaji wa kiima.
Downloads
Published
How to Cite
Issue
Section
Copyright (c) 2017 Joseph Wanyonyi Mulalu

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.
This open-access article is distributed under a Creative Commons Attribution (CC-BY-NC-SA) license.
You are free to: Share — copy and redistribute the material in any medium or format.
Adapt — remix, transform, and build upon the material for any purpose, even commercially. The licensor cannot revoke these freedoms as long as you follow the license terms.
Under the following terms:
Attribution — You must give appropriate credit, provide a link to the license, and indicate if changes were made. You may do so in any reasonable manner, but not in any way that suggests the licensor endorses you or your use.
No additional restrictions You may not apply legal terms or technological measures that legally restrict others from doing anything the license permits.